TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Thursday, January 28, 2016

AFANDE MACHEMBA AWATOA MACHOZI KWA UCHUNGU WAKAZI WA KANDA YA ZIWA, WASEMA KIPAJI ANACHOKIONESHA WANAKUMBUKA MAREHEMU STEVEN KANUMBA ALIVYOWEZA KUITANGAZA NCHI KIMATAIFA..!

 Afande Machemba katika ubora wake akiwa kwenye picha ya pozi dakika chache kabla ya kuingia Location kukamua kwenye moja ya filamu alizoshirkishwa hivi karibuni huko Mkoani Arusha mara baada ya kupokea mwaliko toka kwa wasanii wa huko wakimtaka akacheze filamu.
  Afande Machemba
 Marehemu Steven Kanumba ambae ni kabila moja na Afande Machemba wote ni Wasukuma.
Na Mwandishi Wetu-Mwanza
Msanii Kinda toka kiwanda cha filamu za Kitanzania Joseph Machemba ameendelea kuwa gumzo nchini na safari hii mashabiki wa filamu toka Kanda ya Ziwa wamejikuta wakibubujikwa na machozi mara wanapoongalia filamu alizocheza msanii huyo toka Shinyanga ambae kwa sasa amehamishia makazi yake Jijini Dar huku wengi wakimfananisha na Marehemu Kanumba.
Mmoja wa wadau wa filamu Mkoani Mwanza aliyejitambulisha kwa jina la Majiha Mankunga alisema' Jamani tunamshukuru Mungu kwa kutupoza machungu tuliyoyapata miaka kadhaa iliyopita kwa kuturudishia mtu mwingine muhimu kwetu, huyu Afande Machemba hakika ni kama Kanumba amezaliwa upy" Alisema mtu huyo ammbae ni msambazaji wa filamu za kitanzania kanda ya ziwa
Msanii Joseph Machemba ambae kwa sasa anatamba kwenye filamu za Bifu la Kitongoji na Filamu ya AKIRI NYINGI ambazo ndani yake msanii huyo ameonesha uwezo wa ajabu kiasi cha kuwashangaza mastaa mbalimbali wa bongo movie kwa kipaji alichokuwa nacho Afande Machemba, Huku watanzania wengi wakimtakia kila raheli msanii huyo kwa juhudi zake

Saturday, January 23, 2016

WACHUNGAJI, MASHEKH WAWACHARUKIA RAIS MAGUFULI, DC MAKONDA NA LUKUVI, WAFUNGA SIKU 40, WASEMA MUNGU ATAKACHOWAFANYIA ULIMWENGU UTAJUA...!

     
DC Paul Makonda akiwa kwenye  kutimiza majukumu yake ya kazi huko Nyakasangwe  huku akipongezwa kwa kazi nzuri ya usuruhishi anayoifanya, ambapo makanisa yote pamoja na Mashekh wameungana kufanya maombo ya siku 40 kwa DC huyo, Waziri Lukuvi pamoja na Rais Magufuli ili Mungu azidi kuwafungua wamalize mgogoro wa Ardhi wa kata ya Nyakasangwe na Nyakalekwa zote zikiwa kata ya Wazo ikiwemo na kuwaombea marehemu waliuawa kwenye mgogoro huo miaka miwili iliyopita wakiwemo mabaunsa waliopigwa mishare ya shingo na kichwani.
Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli ambae yupo kwa sasa yuko chini ya maombi makali toka kwa watumishi hao wa Mungu pamoja na wakazi wa Wazo ili afanye maamuzi madogo tu yatakayoondoa ufisadi huo wa ardhi wa watu wenye fedha nyingi wanaodai ni mashamba yao waliyokuwa wameyatelekeza zaidi ya miaka 25, hadi Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Makamba alipoamuru wananchi wapewe mapori hayo yaliyokuwa yanaficha majambazi sugu.
                                  
Waumini wa Kanisa la Hosana lililopo chini ya mchungaji Mzola wakiwa kwenye maombi maalum ya siku 40 kwa Dc Makonda na Waziri Lukuvi pamoja na Rais ili Mungu awafungue wawezi waweze kumaliza tatizo hilo linaloonekana ndani yake lina ufisadi wa kutisha huku baadhi ya watu wa mipango miji na Ardhi Kinondoni wakilalamikiwa kuhusika.
Waumini wa Kanisa la Hosana lililpo Nyakasangwe wakimlilia Mungu ili amfungulie Rais wa Magufuli na Waziri wa Ardhi ili awadhibu mafisadi ardhi walisababisha mauji ya wananchi wa eneo hilo kwa vile mgogoro huo unaneshwa dhahiri una umfisaidi ndani yake.

 
 Mmoja wa wazee wa Kanisa la Hossana akiwa kwenye hisia kali ya maombi kwa Mungu

 Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Hosana Mch Mzola
 Waziri wa Ardhi Mh Lukuvu kwa sasa yupo chini ya maombi hayo ili afanye maamuzi sahihi.
 Mchungaji Amos Mbena Mchungaji Mkuu wa Kanisa  la Pentecostal Holness Mision lililopo Kimara lakini mchungaji huyo amekuwa akiguswa sana na mgogoro huo hivyo nae ameungana kuongeza nguvu ya maombi ili viongozi hao wasikie kilio cha wananchi hao.
Shkhe Sharif Khamis kijana mwenye nguvu ya ajabu kwenye maombi nae ameungana na watumishi hao mbalimbali na wananchi kwenye maombi ya kumaliza mgogoro wa ardhi wa eneo hilo.
Wakina mama na watoto ambao kwa sasa wanaishi mazingira magumu baada ya nyumba zao kubomolewa na polisi kwa shinikizo la mafisadi, wakimlilia Mungu wao.

Na Mwandishi wa Maskanibongo Gazeti
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda, Rais Magufuli na waziri wa Ardhi Mheshimiwa Lukuvu wapo chini ya maombi makali ya siku 40.
Wakazi wa Kata ya Wazo kwenye Mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa wakishirikiana na mashekh na wachungaji wameanzisha maombi hayo maalum kwa ajiri ya Mungu kuwafungua viongozi hao ili wamalize mgogoro huo ndani yake wenye harufu ya rushwa na ufisadi huku maafisa Ardhi na watu wa Mipango Miji Manspaa ya Kinondoni wakitajwa kuhusika.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wachungaji wa makanisa yaliyopo Mitaa ya Nyakasangwe na Nyakalekwa walisema" Tupo kwenye maombo haya ili Mungu awafungue viongozi wetu kwa vile wao ndiyo wenye mamlaka ya mwisho wamalize hili jambao kwani tunaamini Tanzania kwa sasa imepata rais ambae watanzania walikuwa wakimuhitaji hivyo tumeona ni vyema tukamlilia Mungu azidi kumfungua zaidi na kuona hata mgogoro uliopo kwenye mtaa wetu " Alisema Mchungaji Mzola
Hata hivyo wachungaji hao waliendelea kusema kuwa kazi kubwa aliyoifanya Mheshimiwa Paul Makonda ni kubwa sana na hakika sasa mahara alipofikia anahitaji nguvu ya maamuzi ya Mheshimiwa Waziri Lukuvi na Rais kwa vile mtandao alioukuta mheshimiwa Makonda kwenye mgogoro wetu ni mkubwa na inaelezwa ndani yake kuna baadhi ya vigogo wa Ardhi Manspaa.
Wakazi hao waliendelea kusema Mheshimiwa Makonda amediliki kuhatarisha maisha yake kwa kupigania haki ya wananchi licha ya kwamba amekuwa akikutana na vikwazo kutokana na kuzungukwa na watu ambao hawapo upande wake bali wakiwa upande wa mafisadi hivyo sasa ni zamu ya Waziri kumpa meno ya yenye makali kumaliza mgogoro huo kwa kutoa maamuzi yatakayoondoa kabila mgogoro huo.
Mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa inaongozwa na Mwenyekiti wake Peter Bilebela ambae amekuwa kipenzi cha wakazi hao kutokana na utendaji wake wa hali na kuogpa rushwa kama ukoma, hali hiyo imepelekea kuchukiwa na upande wa pili wa mafisaidi kiasi cha kumtengenezea zengwe kila kukicha kwa kutumia pesa waliyokuwa nayo

Friday, January 22, 2016

HATARI YA NJAA MPWAPWA DODOMA: WANANCHI WASHINDIA MBOGA ZA MAJINI KUNUSURU MAISHA YAO, WAMTOLEA UVIVU MBUNGE WAO MWENYE TABIA YA KUKAA KIMYA BUNGENI, WAMTAKA ASIONE AIBU AOMBE MSAADA ILI KUOKOA MAISHA YAO, PICHA HIZI HAPA....!


WANANCHI WA MPWAPWA KIJIJI CHA MAKUTUPA KAMA WALIVYOKUTWA NA CAMERA ZA MASKANIBONGOTZ WAKIANDAA MBOGA ILI WACHEMSHE WAPATE KULA AMBAPO HALI YA JAA IMEKUWA TISHIO KUTOKANA NA MWAKA JANA MVUA KUSHINFWA KUNYESHA, AMBAPO WANANCHI HAO WAMEMTAKA MBUNGE WAO MHESHIMIWA GEORG LUBELEJE KUACHA KUKAA KIMYA BUNGENI AZUNGUMZE UKWELI KUHUSU HALI YA NJAA JIMBONI KWAKE ILI WAPATE MSAADA
 MHE: GEORG LUBELEJE  AMEOMBWA KUACHA TABIA YA KUKAA KIMYA BUNGENI BADALA YAKE APAZE SAUTI NA KUELEZA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOLIKABIRI JIMBO LAKE IKIWEMO NJAA NA UMASKINI ULIOKITHIRI HUKU WANANCHI WENGI WAKIHITAJI MSAADA KWENYE JIMBO LAKE HILO LA MPWAPWA
WAKAZI WENGINE WA KIJIJI CHA  MBORI KATA YA MATOMONDO WAKIPEMBUA MBEGU ZA MABOGA ILI WAFANYE CHAKULA. Na Mwandishi wa maskani bongo gazeti Mpwapwa. Wananchi wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma wamemjia juu mbunge wao mwenye tabia ya kukaa kimya awapo mjengoni na kumwambia asione aibu kusema ukweli kwamba anahitaji msaada wa hali na mali wa chakula ili awanusuru na kifo. Gazeti la Maskani Bongo ambalo lipo Wilaya humo kujonea na hali halisi ya njaa huku watu wengi wakionekana kuhitaji msaada wa hali na mali mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Mabwemazeru aliyejitambulisha kwa jina la Jemsi Luhunga alisema" Ndugu mwandishi kwanza tunawashukuru Maskani Bongo kufika huku kijijini na kujionea balaa la njaa kiukweli hali sio nzuri Serikali isipofanya jitihada za haraka tunaweza kuzungumza mengine"Alisema Nae Mama mmoja mjane toka kijiji cha Lupeta Chang'ombe aliyejitambulisha kwa jina la Mama Emy  alisema" Jamani chonde chonde tunaomba msisitieni Mbunge wengu Lubeleje asikae kimya bungeni kama miaka yote aweke wazi balaa hili la njaa ili Serikali itusaidie tunakufa jamani, asituchukulie sisi kama Mazombi kwa vile tayari yeye tumeshampa kula na familia yake tunachotaka atusaidie kuondoa balaa hili la njaa" Alisema Gazeti hilili lifanya jitihada za kumtafuta Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa ili azungumze jitihada wanazochukua ili kuondoa balaa hilo lakini kwa bahati mbaya hakuwepo ofisini na kudaiwa kuwepo Dodoma mjini.

 

Thursday, January 21, 2016

BONGO MOVIE YAWEKWA CHINI YA ULINZI MKALI NA AFANDE MACHEMBA, WATANZANI WASEMA AFANDE HUYO PEKEE NDIYE ANAEWEZA KUVAA VIATU VYA MAREHEMU KANUMBA..!

 Afande Machemba akiwa mzigoni ambapo Watanzania wengi wamefurahishwa na kipaji cha msanii huyo toka Kanda ya Ziwa ambae kwa sasa amehamishiwa jeshi lake Jijini Dar ili kuikomboa tasnia hii ya filamu ambayo hadi sasa imebaki na wauza sura tu.
Afande Machemba akiwa kwenye moja ya sinema zake
Afande Machemba akiwa kwenye majukumu yake kikazi

Na Mwandishi Wetu
Matumaini ya watanzania yaliyokuwa yamepotea baada ya msanii aliyekuwa na uchungu na Tanzania pamoja na Tasinia ya Filamu marehemu Steven Kanumba  kuondoka Dunia, hatimae sasa yameanza kurejea baada ya msanii Kinda mwenye kipaji cha ajabu kwenye kuigiza Joseph Machemba maarufa kwa jina la "Afande Machemba" kuonesha anaweza
Msanii huyo mwenyeji wa Kanda ya Ziwa akitoka Mkoa wa Shinyanga kwa sasa ndiye amekuwa habari ya mjini kwenye tasnia ya filamu baada ya kuonesha uwezo wa kipekee kwenye moja ya filamu zake alizoshirikishwa ambapo zote zipo mtaani kwa sasa.
Filamu alizoonekana Afande Machemba ni pamoja na, Karoge  Tena, Night Dress, Akiri Nyingi, Siku Moja na nyinginezo nyingi.
Katika filamu hizo msanii huyo ameonesha kama anakipaji na anataka kuifisha tasnia hiyo kimataifa.
Akiongea na mwandishi wetu msanii huyo mpole na asiye na majivuno alisema " Kaka nawashukuru Watanzania kwa kunipokea kwa kweli kazi za mikono yangu zinapendwa sana ambapo hadi sasa watanzania wamenielewa nini ninachotaka kuwafanyia au kuifanyia nchi hii kimataifa hivyo waniunge mkono tu, lakini pia kwa sasa tayari nimepata mtu wa kunisimamia ambae ni mdau Livingstone Mkoi ambapo hadi sasa tayari ameanza kuniwekea mikakati ya kuwa Afande Machemba mwingine" Alisema

HALI YA MSANII MANAIKI SANGA KIMAISHA INASIKITISHA, SASA ANAPAKIA MATOFARI JAPO APATE HELA YA KULA, MASKANIBONGOTZ LAMNASA LIVE..!

Msanii wa Filamu na magizo Manaiki Sanga akipatakia matofari huko Wazo kwa ajiri ya kujipatia ridhiki, ambapo imedaiwa kufuria kwa msanii huyo kumetokana na kuwapanga mademu kama ndoo bombani.
Kajala Masanja ametajwa kwenye kashfa ya kufilisika msanii Manaiki Sanga, huku watu wengi wakisema Kajala anatakiwa kutomtupa Manaiki kwa vile aliwahi kumsaidia vitu vingi kwenye sanaa.

Wednesday, January 20, 2016

USHIRIKINA: MWANAMKE AKUTWA KWENYE PAA LA JENGO LA WIZARA TA FEDHA AKIWA MAZINGIRA YA KUTATANISHA, WAFANYAKAZI WAGOMA KUINGIA NDANI KWA HOFU YA KULOGWA, PICHA HIZI HAPA...!


Manamke ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiwa amekaa juu ya paa la majengo ya Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam leo.


Mwanamke huyo akizungumza na watu waliokusanyika lakini alikuwa hasikiki vizuri maneno aliyokua akiongea kutokana na wananchi waliokusanyika kumuuliza maswali mengi kwa wakati mmoja. 
 

Polisi akiwa pembeni ya uzio wa majengo ya wizara ya fedha na mipango mara baada ya mwanamke huyo kuwa juu ya paa la nyumba hizo. Baada ya muda wafanyakazi wa wizara hiyo walimwekea ngazi na kumshusha ili kumhoji zaidi nini kimemfanya apande juu ya paa la majengo hayo.

WABUNGE CCM WAJIKOKI KUWAKABIRI UKAWA BUNGENI, LITAKUWA NI BUNGE LA KIHISTORIA..!




Tuesday, January 19, 2016

DC MAKONDA, WAZIRI LUKUVI WASHIKWA PABAYA, TAKUKURU KINONDONI YACHAFUKA, NUSRA WASABABISHE MAUAJI, NI BAADA YA AFISA WAKE ASIYYEKUWA MUADILIFU KUMPIGA VIBAYA MWANANCHI NUSU YA……..!

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Simon Sirro
 mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyakasangwe Peter Bilebela aliyekaa karibu na Mh Paul Makonda ambae anazungumza na wakazi wa eneo hilo.

Huyu ndiye mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyakasangwe Peter Bilebela akiwa kwenye moja ya majukumu yake na wananchi hivi karibuni

 Na Mwandisahi wa Maskanibongo gazeti
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kushtua  hali ya utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na Waziri wa Ardhi Mheshiwa Lukuvi la kutaka maeneo yote yenye migogoro yapimwe ili kupata ufumbuzi wa mizozo hiyo inayoendelea Jijini , lakini kwa Kata ya Wazo hali imekuwa tofauti baada ya zoezi hilo kuonekana kuwa na dalili zote za kuvurugwa ili likwame.
Habari zaidi zilieleza kuwa  mgogoro huo wa Wazo mtaa wa Nyakasangwe umekuwa na mitihani mingi hasa kwa viongozi wa Serikali ya Mtaa huo unaongozwa na Mwenyekiti wake Peter Bilebela “Mchungaji”  Kwani mgogoro huo unaohusisha watu wenye fedha nyingi ambao hujiita wenye mashamba na wananchi ambao wanaoitwa wavamizi huku nyuma yake kukiwa na masirahi ya baadhi ya vigogo wazito.
Tukio la jana la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Mtaa huo Peter Bilebela na watu waliofika ofisini kwake huku mwenyekiti huyo akiwa kwenye majukumu yake ya kikao na wajumbe huku watu hao wakijitambulisha kama wao ni maafisa TAKUKURU bila kuonesha vitambulisho.
Akiongea kwa masikitiko makubwa Mwenyekiti  mbele ya Kamanda Mkuu  wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni wakati akihojiwa mara baada ya kufikishwa kwenye Ofisi za Takukuru zilizopo Magomeni Mapipa Jijini Dar es Salaam alisema maafisa hao waliokuwa wametumwa kumkamata walitumia ubabe mkubwa na nguvu nyingi kuliko hekima na ustaarabu kwa kumpiga mbele ya watu.
Mwenyekiti huyo aliendelea kumueleza Mkuu huyo wa Takukuru ambapo Maskanibongo ilifanikiwa kunasa mazungumzo hayo ambapo mwenyekiti huyo alimueleza kamanda huyo kuwa mara baada ya vijana hao kufika ofisini kwake walianza kumkamata mjumbe wake wa Serikali ya mtaa aliyefahamika kwa jina la Mohamed Mangundungundu .
Baada ya kumkata mjumbe huyo aliyekuwa amekaa nje ya ofisi kisha wakamfata Mwenyekiti ambae alikuwa kwenye kikao na kumtaka atoke nje ili apande kwenye gari, lakini mwenyekiti huyo aliwaambia kwamba kuna nini na wao ni akina nani lakini mmoja wa maafisa hao ambae hakufahamika jina lake na ndiye aliyelalamikiwa mwenye matege ya mikono kama baunsa alimjibu mwenyekiti kuwa  yeye hana sababu ya kujitambulisha wala kutoa kitambulisho anatakiwa kupanda gari watafahamiana huko wanakokwenda.
Hali hiyo ilianza kukusanya umati wa watu ambapo kiukweli kitendo cha maafisa hao kutotumia maarifa na akili kutimiza majukumu yao kingeweza kusababisha maafa kwani wananchi wengi walijua ni majambazi wamekuja kumteka mwenyekiti hao hivyo wananchi walishajipanga kwa mapambano na tayari vijan waliashaasha kuchukua silaha za jadi ili kuwakabili watu hao .
Hata hivyo wakati wananchi wakitafakari  juu ya watu hao walikuwa wamegoma kujitambulisha wala kuonesha vitambulisho awari afisa huyo mwenye matege mikononi alimpiga mwenyekiti huyo kibao cha uso hadi miwani kumdondoka huku akimvutia kwenye gari na kufanikiwa kumingiza ndani hapo ndipo walipojitambulisha kama wao ni maafisa wa Takukuru lakini hawakuonesha vitambulisho.
Kabla ya gari hiyo kuondoka wananchi mbali mbali waliokuwa wamefika ofisini pale kupata huduma waliwahoji kwa umakini huku watu maafisa na kuwabana kwa nini wanampiga mwenyekiti huyo ambae alikuwa anabishana nao kimaswali ya msingi ya kutaka wajitambulishe tu basi angeweza kutii, ndipo maafisa hao walipojibu kuwa wao wametumwa kumkamata na kumpiga na mkuu wao ambae ni Kamanda wa TAKUKURU Kinondoni kisha wakawasha gari na kuondoka kwa mwendo wa kasi ya ajabu.
Kimsingi tukio hilo liliwashtua watu wengi ambapo kama si rehema za mungu huwenda lingeweza kuleta maafa kitendo cha maafisa hao kushindwa kutoa vitambulisho mapema na kushindwa kujitambulisha halikuwa jema kwani katika eneo hilo kuna vita inaendelea kati mgogoro wa ardhi kati ya matajiri na wananchi hivyo wananchi wengi walidhani kuwa watu hao ni watekaji kwa jinsi pia walivyokuwa wanatumia ubabe na nguvu nyingi bila hakiri.
Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ambae pia ni mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu  aliyejitambusha kwa jina la Liberty Msuya alisema “ Ndugu mwandisahi  naweza kusema Mungu kasaidia unauona umati huu watu zaidi ya 800 wamekusanyika nusu saa tu na walikuja hapa kwa baada ya kusikia mwenyekiti wao katekwa na watu wasiofahamika sasa je unadhani wangewakuta hapa nini kingetoa unadhani wangetoka salama wangewezaje kupambana na nguvu hii ya uma? “ Alisema mtoto huyo wa waziri na kushauri kuna haja ya watumishi wa namna hiyo kupewa elimu sahihi jinsi ya kukamata watuhumiwa wao kutoa kitambulisha ni usalama wa kwanza kwao.
Hata hivyo baada ya  wananchi kusikia mwenyekiti wao ameshaondoka umati huo uliekea kituo cha polisi Wazo na kuzajana pale kwa ajiri ya kumuulizia kiongozi wao ambapo maafisa wa ngazi za jauu wa kituo hicho walifanyakazi ya ziada kuwaeleza kama kiongozi wao hayupo na wala hawana taarifa za kukamatwa kwao, licha maafisa wa Polisi kuwauliza kama waliokuja kuwamata walitoa vitambulisho? Lakini ilionekana hawakutoa huku Polisi nao wakiingia hofu huenda mwenyekiti huyo alikuwa ametekwa na wahuni na kuwataka waende kituo cha Polisi Oysterbay.
Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mtaa ambao hawakuwepo eneo la tukio ambapo walimpigia RPC Kinondoni simu na kumueleza tukio hilo ambapo alisema kama watu hao walikuwa wametaja kama wao ni Takukuru  labda waende ofisi zao ndipo walipokwenda na kumkuta akiwa chumbani akihojiwa na maafisa wa ngazi za juu wa Takukuru Kinondoni.
Hata hivyo wananchi mbalimbali wakazi wa kata hiyo ya Wazo wamelani vikali tukio la kudhalilishwa kwa kupigwa mwenyekiti wao mbele ya watu kuhusu suala ya kukamatwa wanasema hawaingilii kwa kama kiongozi wao alikamtwa kwa ajiri ya uchunguzi wa hilo hawapingi kwa vile chombo hicho kina haki na mamlaka ya kufanya hivyo, ila tu kitendo cha kushindwa kuonesha vitambulisho vyao na kumpiga ndicho kimepelekea wao kushikwa na tahamaki kwani awali walijua ametekwa na watu huenda waliokuwa wametumwa na wenye mashamba ili wakamdhuru.
Hali hiyo kiukweli ingeweza kuleta maafa makubwa kwa jinsi staili waliyoitumia kumkamata kibabe mwenyekiti huyo kama kundi lile la watu wangekuwepo  tungeweza kuwakosa maafisa wetu hao wa Takukuru ambao ni muhimu kwa taifa letu hasa kipindi hichi cha kutumbua majibu, hivyo ni heri maafisa hao  baadhi wa Takukuru Kinondoni wakaendelea kupewa elimu au kurudi kwenye mafunzo upya kwa ajiri ya kupata maadili ya kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ili kuepuka mdhara kwani hasira waliyokuwa nayo wananchi wa Wazo hakika wangeweza hata kuwachoma moto maafisa hao  kwani wasingeweza kuona mwenyekiti wao akipigwa mbele yao.
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Kamanda Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni ili azungumzie sababu za kumatwa kwa Mwenyekiti huyo ambae alikamatwa akiwa kwenye kikao ofisini  jana tarehe 18 saa kumi jioni na kufikisha makao makuu ya Takukuru ziligonga mwamba mara baada ya simu yake kuita bila kupokelewa hadi habari hii inakwenda mitamboni.
Hata hivyo kitendo cha afisa takukuru huyo kushindwa kutumia akili na maarifa  kwenye utendaji wa kazi yake watu huku akisema katumwa na kamanda mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni ampige mwenyekiti huyo kimetafriwa kama ni kukichafua chombo hicho Mkoa wa Kinondoni kwani haiaminiki kama kweli Kamanda huyo anaweza kumtuma afisa wake ampige mtu asiyekuwa na ubishi, bali itakuwa ni utovu wake wa nidhamu.