TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, April 1, 2016

HIVI NDIVYO UKIMWI UNAVYOWAMALIZA WAFANYAKAZI KITUO CHA MABASI UBUNGO,WAFANYAKAZI WA KIKE WAONGOZA KWA MAAMBUKIZI, , ROBO TATU YA WASICHANA MAAJENTI NI WAATHIRIKA, MUHANGA MWENZAO ATOA SIRI NZITO PIA WAPO WANAOTEMBEA NA MABOSI ZAO KWA SIRI...!



Na Waandishi wa Maskanibongotz/ Sadiktv
Katika hali ya kushtua mtandao huu wa Maskanibongotz umepokea taarifa za kushtua juu ya kuwepo kwa hali ya hatari kwenye Kituo cha Mabasi Ubungo kufuati kuwepo kwa maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi huku wahanga wakubwa wakiwa ni baahi ya wanawake wanaojihusisha na  ukataji tiketi maaraufu kama mawakala na maajenti.
Kikosi cha waandishi wetu wa habari za uchunguzi baada ya kupata taarifa hizo waliamua kufunga safari hadi ndani ya kituo hicho cha  kikubwa na chenye umaarufu mkubwa Afrika Mashariki na nje kutokana na kutoa na kupokea mabasi yanayokwenda nchi mbalimbali Afrika.
Mara baada ya waandishi wetu kutua kituoni hapo walikutana na  mtoa habari wetu ambae ni Dada mwenye maambukizi ya Ukimwi jina linahifadhiwa kama anavyoonekana pichani ambapo aliwakalisha waandishi wetu kitako na kuwaeleza ishu nzima jinsi ukimwi ulivyotapakaa huku waathirika wakubwa wakiwa ni wanawake huku ikidaiwa karibia robo tatu ya wasichana wanaonekana hapo ni waathirika.
Dada huyo ambae ni mwenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro alisema alianza kazi ya ukatishani tiketi tangu mwaka 2006 hadi kampuni anayofanyia kazi mabasi yake yanakwenda Mikoa ya Arusha na Moshi na hata maradhi ameyapata hapo hapo akiwa kazini.
Akiongea kwa majonzi makubwa Dada huyo ambae ana watoto waweili ambao bahati nzuri aliwazaa kabla hajakutwa na janga hilo alisema" Ndugu zangu hali ya hapa ni mbaya ukimiwi umesambaa kama upepo, msione mabinti wamenona hivyo na kujazia hivi wote hapa tuna VVU mimi nisema ukweli tu hata nikificha haisaidii, mfano chumba no****** hao wadada wote mabonge wameshaathirika" Alisema  Dada huyo kwa muonekano wa macho kamwe huwezi amini kama ni mgonjwa
Msichana huyo aliendelea kusema " Sababu kubwa inayotuponza ni tamaa kwani kama mnavyojua hapa wanakuja watu wa kila aina tena wenye madini ya kutosha hivyo ni rahisi mtu kuingia kwenye mtego, lakini wapo wasichana wengine wanatembea na mabosi zao ambao ni wamiliki wa mabasi na wamewafanya nyumba ndogo zao huku majumbani kwao wakiwa na wake zao halali hivyo hali hiyo inapelekea maambukizi kusambaa kwenye familia zao" Alisema
Hata hivyo mdada huyo alisema kuwa kikubwa tamaa tu ndiyo inawaponza kwani kama pesa wana pata sana kwenye kazi zao halali za uajenti huku wengi wakishiri michezo ila tamaa za mwili kuwa mpenzi zaidi ya mmoja ndiyo pia inachangia, na pia kutokana na urembo wa maajenti hao huku wengi wao wakiwa mshalaah pia abiria wengi wanapokuja kukata tiketi hunasa kiulaini.
Dada huyo alimalizia kutoa ushauri wake " Kaka tunaomba kupitia habari hii vyombo vinavyohusika kuelimisha kufika hapa Ubungo terminal kwa ajiri ya kutoa elimu la sivyo miaka 10 mbele watu wengi tutakuwa tumeondoka duniani, Mimi najua ni wa kuondoka leo kesho licha ya kwamba nimeanza dozi lakini najua nitakufa hivi karibuni sitokuwa na maisha marefu" Alisea dada huyo kwa masikitizo
Hata hivyo mtandao huu pia ulibata bahati ya kuongea na mpiga debe mmoja ambae nae pia aliomba hifadhi ya jina lake lakini alikuwa na haya ya kusema" Jamani ndugu waandishi Ubungo inatisha kwa maambukizi yani mfano ikitokea labda kila chuamba cha ofisi watu wakapimwa majibu mtakayoyapata hapa Tanzania itatikisika, na sasa kwa vile tupo wanaume na wanawake hivyo wengi wanatembea pamoja kwa kushiriki tendo la ndoa huku pembeni wakiwa na wapenzi wengine hali inayoongeza maambukizi" Alisema
Mtandao huu unashauri mamlaka zinazohusika na kuelimisha kuhusu gonjwa hili kufanya ziara za mara kwa mara kituoni na kutoa elimu kwani la sivyo tuapoteza nguvu kazi kubwa ya Taifa.
Source Maskanibongotz

No comments:

Post a Comment