TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Saturday, February 6, 2016

UKAWA DAR WAMPIGIA SALUT DC MAKONDA, WAMTAKA AGOMBEE UBUNGE KUPITIA CHAMA CHOCHOTE WATAMPIGIA KURA ZA KUMWAGA, MASKANIBONGOTZ INASHUKA NAYO.....!

DC MAKONDA KATIKATI AKIWA NA MWENYEKITI WA CHADEMA MH MBOWE HIVI KARIBUNI KWENYE MAJUKUMU YA KITAIFA.

Na Mwandisahi wa Maskanibongotz
Wafuasi wengi wa Ukawa Kinondoni Jijini Dar wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda kwa kazi nzuri anayoifanya ya kupambana na ufisadi na kuwa mtetezi wa wanyonge hasa kwenye suara la migogoro ya 
ardhi.
Wakiongea na maskanibongotz  wafuasi hao walianza kusema kuwa" Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni Makonda ni kiongozi anaehitajika kwa watanzania na hata hivyo sijui kwa nini mheshimiwa Rais alichelewa kumteua huenda hata watu wasingepoteza maisha kule Nyakasangwe" Walisema watu hao
Hata hivyo wananchi hao waliongeza kusema kuwa Makonda angepewa Ukuu wa Mkoa wa Dar ili amalize matatizo ya ardhi kabisa kwani hata wilaya nyingine za Jiji la Dar zinamuhitaji kwani alichokifanya Wazo kwenye mtaa wa Nyakasangwe hakika anastahiri pongezi ikizingatia viongozi wengi akiwemo Mkuu wa Mkoa Meck Sadick walishindwa kumaliza tatizo hilo.
Aidha wananchi mbalimbali walitamani hata DC huyo kugombea ubunge Jimbo la Kawe ama Kinondoni ili akapaze sauti yake bungeni.

No comments:

Post a Comment