TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Saturday, January 23, 2016

WACHUNGAJI, MASHEKH WAWACHARUKIA RAIS MAGUFULI, DC MAKONDA NA LUKUVI, WAFUNGA SIKU 40, WASEMA MUNGU ATAKACHOWAFANYIA ULIMWENGU UTAJUA...!

     
DC Paul Makonda akiwa kwenye  kutimiza majukumu yake ya kazi huko Nyakasangwe  huku akipongezwa kwa kazi nzuri ya usuruhishi anayoifanya, ambapo makanisa yote pamoja na Mashekh wameungana kufanya maombo ya siku 40 kwa DC huyo, Waziri Lukuvi pamoja na Rais Magufuli ili Mungu azidi kuwafungua wamalize mgogoro wa Ardhi wa kata ya Nyakasangwe na Nyakalekwa zote zikiwa kata ya Wazo ikiwemo na kuwaombea marehemu waliuawa kwenye mgogoro huo miaka miwili iliyopita wakiwemo mabaunsa waliopigwa mishare ya shingo na kichwani.
Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli ambae yupo kwa sasa yuko chini ya maombi makali toka kwa watumishi hao wa Mungu pamoja na wakazi wa Wazo ili afanye maamuzi madogo tu yatakayoondoa ufisadi huo wa ardhi wa watu wenye fedha nyingi wanaodai ni mashamba yao waliyokuwa wameyatelekeza zaidi ya miaka 25, hadi Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Makamba alipoamuru wananchi wapewe mapori hayo yaliyokuwa yanaficha majambazi sugu.
                                  
Waumini wa Kanisa la Hosana lililopo chini ya mchungaji Mzola wakiwa kwenye maombi maalum ya siku 40 kwa Dc Makonda na Waziri Lukuvi pamoja na Rais ili Mungu awafungue wawezi waweze kumaliza tatizo hilo linaloonekana ndani yake lina ufisadi wa kutisha huku baadhi ya watu wa mipango miji na Ardhi Kinondoni wakilalamikiwa kuhusika.
Waumini wa Kanisa la Hosana lililpo Nyakasangwe wakimlilia Mungu ili amfungulie Rais wa Magufuli na Waziri wa Ardhi ili awadhibu mafisadi ardhi walisababisha mauji ya wananchi wa eneo hilo kwa vile mgogoro huo unaneshwa dhahiri una umfisaidi ndani yake.

 
 Mmoja wa wazee wa Kanisa la Hossana akiwa kwenye hisia kali ya maombi kwa Mungu

 Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Hosana Mch Mzola
 Waziri wa Ardhi Mh Lukuvu kwa sasa yupo chini ya maombi hayo ili afanye maamuzi sahihi.
 Mchungaji Amos Mbena Mchungaji Mkuu wa Kanisa  la Pentecostal Holness Mision lililopo Kimara lakini mchungaji huyo amekuwa akiguswa sana na mgogoro huo hivyo nae ameungana kuongeza nguvu ya maombi ili viongozi hao wasikie kilio cha wananchi hao.
Shkhe Sharif Khamis kijana mwenye nguvu ya ajabu kwenye maombi nae ameungana na watumishi hao mbalimbali na wananchi kwenye maombi ya kumaliza mgogoro wa ardhi wa eneo hilo.
Wakina mama na watoto ambao kwa sasa wanaishi mazingira magumu baada ya nyumba zao kubomolewa na polisi kwa shinikizo la mafisadi, wakimlilia Mungu wao.

Na Mwandishi wa Maskanibongo Gazeti
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda, Rais Magufuli na waziri wa Ardhi Mheshimiwa Lukuvu wapo chini ya maombi makali ya siku 40.
Wakazi wa Kata ya Wazo kwenye Mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa wakishirikiana na mashekh na wachungaji wameanzisha maombi hayo maalum kwa ajiri ya Mungu kuwafungua viongozi hao ili wamalize mgogoro huo ndani yake wenye harufu ya rushwa na ufisadi huku maafisa Ardhi na watu wa Mipango Miji Manspaa ya Kinondoni wakitajwa kuhusika.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wachungaji wa makanisa yaliyopo Mitaa ya Nyakasangwe na Nyakalekwa walisema" Tupo kwenye maombo haya ili Mungu awafungue viongozi wetu kwa vile wao ndiyo wenye mamlaka ya mwisho wamalize hili jambao kwani tunaamini Tanzania kwa sasa imepata rais ambae watanzania walikuwa wakimuhitaji hivyo tumeona ni vyema tukamlilia Mungu azidi kumfungua zaidi na kuona hata mgogoro uliopo kwenye mtaa wetu " Alisema Mchungaji Mzola
Hata hivyo wachungaji hao waliendelea kusema kuwa kazi kubwa aliyoifanya Mheshimiwa Paul Makonda ni kubwa sana na hakika sasa mahara alipofikia anahitaji nguvu ya maamuzi ya Mheshimiwa Waziri Lukuvi na Rais kwa vile mtandao alioukuta mheshimiwa Makonda kwenye mgogoro wetu ni mkubwa na inaelezwa ndani yake kuna baadhi ya vigogo wa Ardhi Manspaa.
Wakazi hao waliendelea kusema Mheshimiwa Makonda amediliki kuhatarisha maisha yake kwa kupigania haki ya wananchi licha ya kwamba amekuwa akikutana na vikwazo kutokana na kuzungukwa na watu ambao hawapo upande wake bali wakiwa upande wa mafisadi hivyo sasa ni zamu ya Waziri kumpa meno ya yenye makali kumaliza mgogoro huo kwa kutoa maamuzi yatakayoondoa kabila mgogoro huo.
Mtaa wa Nyakasangwe na Nyakalekwa inaongozwa na Mwenyekiti wake Peter Bilebela ambae amekuwa kipenzi cha wakazi hao kutokana na utendaji wake wa hali na kuogpa rushwa kama ukoma, hali hiyo imepelekea kuchukiwa na upande wa pili wa mafisaidi kiasi cha kumtengenezea zengwe kila kukicha kwa kutumia pesa waliyokuwa nayo

No comments:

Post a Comment