TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, February 6, 2015

Rais Wa Ujerumani Asisitiza Jambo Afrika Mashariki


rais wa Ujerumani Bw. Joachim Gauck amezitaka  nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kuimarisha ushirikiano miongoni mwao. Ushirikiano huo  unahusisha  kukabiliana na changamoto  zilizopo  pamoja  na kuimarisha misingi ya haki za binadamu.
Aidha, Bw. Gauck amesema hayo baada ya kuhitimisha ziara yake hapa nchini kwa kutembelea makao makuu ya mahakama ya afrika inayoshughulikia haki za binadamu na jumuiya ya Afrika Mashariki zote zilizoko jijini  Arusha.
Naye  Rais wa mahakama ya Afrika jaji mstaafu Agustino Ramadhani na katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Dr. Richard Sezibera wamesema ziara hiyo imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano na  imeongeza chachu ya maendeleo.
Kwa upande mwingine  Rais huyo amemaliza ziara yake nchini Tanzania  kwa kutembelea hifadhi ya taifa ya Serengeti ikiwa ni kuhamasisha watalii kutoka nchini Ujerumani.

No comments:

Post a Comment