TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, October 13, 2014

TBREAKING NEWS: RAFIKI APIGWA VIBAYA NA WANANCHI UBUNGO JIJINI DAR, ALIPIGWA MTAMA ULIOMPAISHA KIMO CHA NG'OMBE..!



Wananchi  wenye ghazabu kali wamemshambulia  kwa ngumi na mateke kisha kumkamata askari wa usalama barabarani  asiyefahamika jina lake maeneo ya Ubungo - Dar es Salaam baada ya kusababisha ajali.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, askari huyo alisababisha ajali hiyo wakati akiongoza magari baada ya kuita magari kutoka pande mbili kwa wakati mmoja, ambapo baada ya kuona wamechoka muda mrefu  kwenye foleni baadhi ya waendesha magari hao walishuka kwenye gari zao na kumfuata kisha kuanza kumshambulia ambapo jamaa mmoja alionekana kumpiga mtama afande huyo na kumpaisha juu kimo cha ng'ombe kisha kudondoka chini.
Hata hivyo afande huyo aliona atoke nduki kwa ajili kuokoa mtima wake lakini hakufika popote ambapo alikamatwa na kuendelea kupigwa ngumi za chembe na kusababisha kushindwa kupumua 
Pichani raia wakimlazimisha askari huyo kuingia kwenye bajaji ili kumfikisha kituo cha polisi.
CREDIT: MASKANIBONGOTZ

No comments:

Post a Comment