TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Wednesday, October 29, 2014

ANGALIA ACHOKIZUNGUMZA MBABEJACKIE CHAN BAADA YA MWANAE KUKAMATWA NA MADAWA NCHINI CHINA..!


JackieMkali wa movie kutoka Hong Kong China, Jackie Chan ameomba vyombo vya habari ‘vijichunge’ na namna vinavyoandika taarifa kuhusiana na kitendo cha mtoto wake kukamatwa na dawa za kulevya kwa kuwa kufanya hivyo si kumuumiza yeye (Jackie Chan) bali ni kumuumiza mama wa mtoto huyo.
Jackie Chan amesema kupitia tukio hilo amejifunza kuwa baba bora kitu ambacho hakukijua siku za nyuma.
Mtoto wa staa huyo, Jaycee Chan alikamatwa kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi zaidi ya gramu 100 ndani ya nyumba yake, na baadaye kushitakiwa kwa kuuza dawa hizo.
Jackie Chan ambaye amekuwa balozi wa kupinga dawa za kulevya tangu mwaka 2009, amesononeshwa na pia ameomba radhi kwa kosa alilotenda mwanae ambapo hii imekuwa mara yake ya kwanza kujibu swali linalohusiana na kesi ya mtoto wake, akisema kupitia hilo amejifunza kuwa baba bora.

No comments:

Post a Comment