TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Saturday, August 16, 2014

WANANCHAMA WA CCMA ZAIDI YA ELFU 200 WATISHIA KUJIENGUA KISA VIONGOZI WA CHAMA NGAZI ZA JUU KUWATELEKEZA HUKU WAKIWANYANYASIKA BILA MSAADA, ANGALIA HABARI HII YA KUSIKITISHA....!


 Abdulrahman Kinana
Nape Nnauye
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kitongoji cha Nakasangwe mtaa wa madale kata ya Wazo ambao ni wanachama wa CCM wametishia kukihama chama hicho endapo uongozi wa CCM Kitaifa hawatawafika kwenye eneo hilo lenye mgogoro wa Ardhi kati ya mwenyezaji na wao.
Wakiongea na waandishi wa habari kituo cha E-FM RADIO hivi karibuni wananchi hao walisema kuwa CCM imewatelekeza bila msaada wowote licha kuwa na taarifa juu ya unyanyasaji wanaofanyiwa na viongozi wa Serikali wa Mkoa wanaodai kuwa anashirikiana na wawekezaji kuwapora ardhi yao.
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha Mama Jasmin alisema" Sisi tunaishi maisha magumu sana awali walikuja na kutuambia sisi si watanzania lakini uchaguzi uliopita tulipiga kura na baada ya hapo tena wakaja kutuvunjia nyumba zetu wakidai tumevamia eneo hilo lakini ukweli hii si haki hata kidogo tunawaomba viongozi wetu wa CCM Nape Nnauye na  Abdulrahman Kinana waje kutusikiliza pamoja na kutusaidia  la sivyo hakika tuko tayari kuhama chama" Alisema mama huyo
Kata hivyo imekuwa ngome ya CCM miaka mingi huku upinzani ukiwa hauna nguvu ambapo hata uchaguzi wa 2010 CCM ilijinyakulia kura nyingi, na ndio maana wananchi wa huko wahawajawah kumfuata mbunge wao Halima Mdee na kumlalamikia matatizo yao.

No comments:

Post a Comment