TANGAZO MAALUM

TANGAZO MAALUM
.

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Monday, August 4, 2014

BAADA YA RIDHIWANI KIKWETE, WEMA SEPETU NAE AMEOMBWA KUMSAIDIA MSANII TINO MADHAHABU ANAHITAJI KUFANYIA UPASUAJI WA NYAMA ZILIZOMUOTA PUANI..!



Na Mwandishi Wetu
Mashabiki mbalimbali wa msanii Wema Sepetu wamemuomba kujitokeza kwa ajili kunusuru maisha ya msanii Tino Madhahabu anaesumbuliwa na ugonjwa pumu pamoja na kuvimba kwa nyama ndani ya pua huku hali yake ikiwa tete.
Wakiongea na Xdeejayz mashabiki hao walisema" Tunaimani kubwa na Wema Sepetu kumsaidia msanii huyo hata kwa kuanzisha harambe maalum ya kuwachangisha watu fedha ili msanii huyo aweze kufanyiwa upasuaji" Alisema Juta B ambe ameguswa sana matatizo ya msanii huyo wa muda aliyewahi kutamba kwa kwenye tv kwenye michezo ya Bongo Dar es Salaam
Aidha mashabiki hao waliongeza kusema ni heri wasanii wote wakaungana kumsaidia msanii mwenzao ili wanusuru maisha yake kuliko kusubiri hatua nyingine ambayo kwa kawaida wasanii huchaguana kwenye kamati na kuchangisha fedha.
Msanii Tino ambae  mwishoni mwa wiki iliyopita alimuangukia Mh Ridhiwan Kikwete kwa kumuomba msaada ili kunusuru maisha yake.
Msanii Tino anapatikana kwa simu namba 0767-250026 na watanzania wote watakaoguswa wajitokeze kumsaidia.

No comments:

Post a Comment