friday

friday

TANGAZA NA SISI

TANGAZA NA SISI KWA BEI NAFUU TUPIGIE KUPITIA 0713 57 57 18 AU TUMA BARUA PEPE DTV@EML.CO.TZ

Friday, October 31, 2014

MGANGA WA MASTAA NCHINI AZUSHA BALAA KUBWA KWA MASHABIKI WA WEMA SEOETU. ALLY KIBA AHUSISHWA..!


 Mganga wa Mastaa nchini pamoja na Diamond akiwa ofisini kwake.

 Na Sakina Shabani
Yule Mganga aliyejipatia jina kubwa nchini Tanzani baada miti shamba zake kuwasaidia watu wengi sana huku vigogo wa Serikali na mastaa wakimtumia kuwekea sawa mambo yao ya mafanikio amezusha balaa kubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuzungumzia mabalaa yanayomkuta mwanamuziki kipenzi cha watu Diamond
.Kwa mujibu wa mtandao wa mganga huyo ambae miti shamba zake zimepelekwa nchi zilizoathirika na ugonjwa wa Ebola kwa ajili ya majaribio alisema kuwa kuanza kuporomoka kwa mwanamuziki Diamond ni dalili za mwisho wa mwanamuziki huyo kimuziki na tayari nyota yake itachukuliwa na mwanamuziki chipukizi ambae hata hivyo hakumtaja jina.
Baada ya taarifa hizo shemeji zake ambao ni mafans wa Wema walianza kumshambulia mganga huyo ambae kwa sasa yupo Jijini Dar kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa Jiji la Dar huku wengi wakimtukana mganga huyo.
Hata hivyo mganga huyo alipotafutwa na gazeti kupitia namba yake ya simu 0788-8444902 alipatikana na kusema" Unajua Diamond na kijana wangu na tumeshiriki kumuinua lakini kwa hali inavyoonekana tayari mwisho wa ustaa wake umefika na dhahiri shahiri mtu mwingine anakuja kukalia kiti chake" Alisema mganga huyo
Aidha mganga huyo ambae amekuwa akitumiwa sana wafanyabishara pia kusafisha mambo yao kutumia miti shamba zake, huku viongozi wa vyama na siasa nao hawaishi nyumbani kwake kupata baraka zake.
Pia anatibu magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana kama uzazi, ganzi miguuni na mikononi, kisukari, Ukimwi kupandisha CD4 kwa wiki moja tu, kumuona mchawi live bila king'amuzi nk. Na ametoa uwito kwa wananchi kuelendelea kuitumia nafasi hiyo kabla hajaondoka msimu huu wa mwisho wa mwaka

WAKATI BONGO MOVIE WAKIOMBOLEZA MSIBA WA MSANII MZEE MANETO, MSANII TINO MADHABU HALI YAKE NI MBAYA ANAHITAJI MSAADA KUNUSURU UHAI WAKE. DUDE ATUHUMIWA KULA HELA ZA MCHANGO..!MSANII TINO MADHAHABU AMBAE TANGU WIKI ILIYOPITA AMEZIDIWA KWA UGONJWA KUOTA NYAMA PUANI HUKU AKIKOSA MSAADA WA WASANII WENZAKE
 http://www.bongomovies.com/public/uploads/R.I_.P_.jpg
 Wakati mashabiki na wasanii wa Bongo Movie wakiomboleza msiba wa Mzee Manento amefariki dunia hapo juz. kuna taarifa kuwa msanii mwingine wa Bongo Movie Tino Madhahabu nae amelazwa huku akitelekezwa bila msaada huku msanii Dude akituhumiwa kula pesa za mchango wa kumuuguzia msanii huyo.
Kwa mujibu chanzo chetu kiliieleza Maskanibongotz kuwa msanii amekuwa akiugua zaidi ya miaka miliwi na hivi karibuni familia ya msanii huyo  ilitoa taarifa kwenye vyombo vya habari kuhusu kuugua kwa  msanii huyo huku wasanii wenzake kumtelekeza ambapo mtandao huu uliwasiliana na Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Saimon Mwakifwamba ambae alikuwa amemuagiza Dude afike nyumbani kwa Tino kwa ajili ya kuangalia hali halisi harafu michango ianze kuchangwa kwa ajili ya kunusuru uhai wa msanii huyo.
Hata hivyo kwa mujibu wa Tino mwenyewe alisema kuwa Dude alipiga simu kwake na kumueleza kama amepata taarifa zake toka kwa Rais hivyo ataendesha harambe ya mchango kisha atafika kwake toka hapo hali leo hajawahi kupiga simu kuelezea hiyo harambe imefikia wapi hali inayotia shaka huenda labda amekula mchango huo.
Maskanibongotz ilimtafuta Dude kupitia simu yake ya kiganjani ili kueleza ukweli wa tuhuma hizo ambapo simu ya msanii huyo iliita tu bila kupokelewa.
CREDIT: MASKANIBONGOTZ

BANK YA NMB YAWAKUNA VIJANA DODOMA, MAELFU WAFURIKA KWENYE BONANZA UDOM, WANACHI WACHANGAMKIA FURSA..!


LEO NDIO KILELE CHA BONANZA HILO LILILOANDALIWA NA NMB TAWI LA UDOMA AMBAPO ITAKUWA NDIO FAINALI YA MPIRA WA MIGUU NA  MIKONO SAMBAMBA YA YOTE HAYO PIA KUTAKUWA NA BURUDANI KUTOKA KWA WASANII MBALI MBALI AKIWEMO BARNABA BOY, BONANZA HILO LITAANZA SAA 8 MCHNA NA KUENDELEA NA HAKUNA KIINGILIO


Wednesday, October 29, 2014

MUZIKI MNENE BAA KWA BAA KUKINUKISHA TEGETA DARAJANI NDANI YA BAA YA KIMORI HIGHWAY PARK. 93.7 E-FM YAZIDI KUTIKISA NCHI WAHESHIMIWA WABUNGE WATOA 5...!


Tarehe 1 Novemba, 2014 ni siku ya kukumbukwa kwa wakazi wa Tegeta Darajani  na vitongoji vyake kufuatia program ya Muziki Mnene baa kwa baa kushusha  bonge la burudani

WALIOMUUA CAPTAIN WA BAFANABAFANA KUTAMBULIWA KITAALAM, MKEWE AELEZEA JINSI WALIVYOMPIGA RISASI HUKU AKIWA NA BUNDUKI YAKE KIUNONI..!

Kelly Kumalo mpenzi wa Senzo akiwa na mtoto wa Senzo Meyiwa.
Polisi nchini Africa Kusini wameonesha nyuso zinazo dhaniwa kuwa ni wauaji wa golikipa na kapteni wa timu ya taifa Africa Kusini Bafana Bafana, Senzo Meyiwa.
Meyiwa alipigwa risasi na kufa siku ya jumapili wakati alipokuwa akikabiliana na wavamizi waloingia nyumbani kwa mpenzi wake Kelly Khumalo ambaye ni mwanamuziki na pia ni muigizaji,maziko ya Meyiwa yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
Kifo cha mwanasoka huyo kimeonesha picha halisi ya kiwango cha uhalifu na matumizi mabaya ya silaha nchini Africa Kusini.
Africa kusini inatajwa kuwa moja ya nchi zenye matukio makubwa ya uhali,na kiwango cha uhalifu kinazidi kuongezeka siku hadi siku.
Mwanzoni mwa mwezi huu mwanariadha Oscar Pistorious alihukumiwa miaka mitano jela kwa kosa la kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake.

ANGALIA ACHOKIZUNGUMZA MBABEJACKIE CHAN BAADA YA MWANAE KUKAMATWA NA MADAWA NCHINI CHINA..!


JackieMkali wa movie kutoka Hong Kong China, Jackie Chan ameomba vyombo vya habari ‘vijichunge’ na namna vinavyoandika taarifa kuhusiana na kitendo cha mtoto wake kukamatwa na dawa za kulevya kwa kuwa kufanya hivyo si kumuumiza yeye (Jackie Chan) bali ni kumuumiza mama wa mtoto huyo.
Jackie Chan amesema kupitia tukio hilo amejifunza kuwa baba bora kitu ambacho hakukijua siku za nyuma.
Mtoto wa staa huyo, Jaycee Chan alikamatwa kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi zaidi ya gramu 100 ndani ya nyumba yake, na baadaye kushitakiwa kwa kuuza dawa hizo.
Jackie Chan ambaye amekuwa balozi wa kupinga dawa za kulevya tangu mwaka 2009, amesononeshwa na pia ameomba radhi kwa kosa alilotenda mwanae ambapo hii imekuwa mara yake ya kwanza kujibu swali linalohusiana na kesi ya mtoto wake, akisema kupitia hilo amejifunza kuwa baba bora.

BREAKING NEWS: UBUNGO KWA WAKA MOTO HOFU NA MASHAKA KWA WANANCHI WAKIMBIA OVYO KUOKOA MAISHA YAO MUDA HUU...!


 Hii ndiyo hali halisi ya tukio muda huu 
Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni Camilius Wambura